1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabul. Wanajeshi wa NATO wauwawa.

15 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD2d

Wanajeshi wawili zaidi wa jeshi la NATO, ambao wametambulika kuwa ni kutoka Canada, wameuwawa na wengine watatu wamejeruhiwa wakati wa mapambano kusini mwa jimbo la Kandahar nchini Afghanistan.

Jimbo hilo limekuwa na mapigano makali katika muda wa miezi michache iliyopita baina ya wapiganaji wa Taliban na majeshi ya NATO.

Kandahar linaonekana kuwa eneo hatari zaidi nchini Afghanistan.

Mwandishi habari wa Italia ameripotiwa kutekwa nyara wiki hii. Shirika la habari la Afghanistan limesema kuwa wapiganaji wa Taliban walisimamisha basi lililokuwa na abiria ambalo alikuwa akisafiria na kuondoka nae.