1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL : Wanajeshi 2 wa NATO wauwawa

15 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD2k

Nchini Afghanistan wanajeshi wawili wa Umoja wa Kujihami wa Mataifa ya Magharibi NATO waliotambulika kuwa ni wa Canada wameuwawa.

Wanajeshi wengine watatu wa NATO wamejeruhiwa wakati wanamgambo walipowashambulia kwa magurunedi yaliyovurumishwa na maroketi pamoja na kushambuliwa kwa risasi. Mapigano hayo yaliodumu kwa zaidi ya masaa matatu yalitokea katika jimbo la kusini la Kandahar.

Katika jimbo la Helmand imeripotiwa kwamba mwandishi wa kupiga picha wa Italia ametekwa nyara.Vitendo vya utekaji nyara kwa sababu za uhalifu na kisiasa vimekuwa vikizidi kuwa vya kawaida nchini kote Afghanistan ikiwa ni miaka mitano baada ya kupinduliwa kwa utawala wa Taliban na uvamizi ulioongozwa na Marekani.