KABUL: Wanajeshi 2 wa NATO wauawa.
7 Juni 2007Matangazo
Askari wawili wa Majeshi ya NATO wameuawa wakati wa makabiliano kati ya majeshi hayo na wanamgambo kusini mwa Afghanistan:
Taarifa ya majeshi hayo imesema askari hao waliuawa jana katika maeneo tofauti wakati majeshi yakipambana na wanamgambo.
Uraia wa wanajeshi hao haujatangazwa .
Mwaka huu pekee, wanajeshi sabini na tisa wameuawa nchini Afghanistan.