KABUL: Vikosi vya NATO vimeua Wataliban 20
13 Oktoba 2006Matangazo
Kiasi ya waasi 20 wameuawa katika mapigano yaliyozuka kusini mwa Afghanistan,kati ya wanamgambo wa Kitaliban na vikosi vya kimataifa ISAF vinavyoongozwa na NATO.Kwa mujibu wa NATO, kama wanamgambo 60 wa Kitaliban waliwashambulia wanajeshi wa ISAF waliokuwa wakipiga doria katika wilaya ya Kandahar kusini mwa Afghanistan. Wanajeshi hao wakafyatua risasi na waliomba msaada wa vikosi vya anga.