KABUL: Shirika la NATO lasema Wataliban 11 wameuawa
23 Agosti 2006Matangazo
Msemaji wa shirika la kujihami la nchi za magharibi NATO amesema,ndege za NATO zimeua si chini ya waasi 11 wa Kitaliban kusini mwa Afghanistan.Akaongezea kuwa kundi la Wataliban 15 liligunduliwa likitayarisha shambulio la uvamizi karibu na barabara kuu kwenye jimbo la Kandahar. Watu hao waliuawa baada ya kukimbilia ndani ya ua wa nyumba moja.Wakazi wa hapo lakini wamesema,wale waliouliwa walikuwa wakulima waliokuwa wakichuma zabibu.Afghanistan hivi sasa inashuhudia mapigano makali kabisa kupata kutokea tangu vikosi vya ushirikiano,chini ya uongozi wa Marekani kuingóa madarakani serikali ya Taliban mwaka 2001.