1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Shirika la NATO lachukua uongozi wa jeshi la kulinda amani

6 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD5f

Shirika la NATO limechukua uongozi wa wanajeshi elfu 12 wa jeshi la muungano lililokuwa likiongozwa na Marekani katika eneo la mashariki mwa Afghanistan. Hatua hii imeiongeza idadi ya wanajeshi wanaofanya kazi katika jeshi la ISAF kufikia zaidi ya elfu 30.

Katika sherehe ya kupewa madaraka mjini Kabul, kamanda wa jeshi la ISAF, jenerali David Richards wa Uingereza alisema wanajeshi hao wa Marekani mashariki mwa Afghanistan watakiongezea nguvu kikosi cha ISAF.

Jenarali Richards, alisema, ´Huu ni wakati wa kupiga hatua mbele. Tutaendelea kukabiliana na wapiganaji wakati wowote na mahala popote kukiwa na haja ya kufanya hivyo. Lakini lengo msingi la operesheni zetu za usalama ni kuiwezesha serikali iongeze uwezo wake na kuharakisha juhudi za kujenga upya na kuleta maendeleo ili kuwafaidi kikweli waafghanistan wote.´