KABUL: Shambulizi la NATO limeua hadi watu 45
22 Juni 2007Matangazo
Shambulio la vikosi vya anga vya NATO,kusini mwa Afghanistan,limeua hadi watu 45.Ripoti za vyombo vya habari zinasema,si chini ya raia 25 ni miongoni mwa wale waliouawa katika shambulizi lililofanywa wakati wa usiku.Inaaminiwa kuwa wengine waliouawa,walikuwa wapiganaji wa Taliban.