1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Shambulizi la kujitolea muhanga limeua hadi watu 50

7 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C79P

Watu wasiopungua 50 wameuawa nchini Afghanistan katika shambulizi baya kabisa kupata kufanywa na wanamgambo wa kujitolea maisha muhanga nchini humo.Miongoni mwa wale waliouawa ni wabunge sita na watoto.Vile vile kama watu 100 wamejeruhiwa. Shambulizi hilo limefanywa,wakati ujumbe wa ngazi ya juu ulikuwa ukitembelea kiwanda cha sukari kilichojengwa kwa msaada wa Ujerumani katika wilaya ya Baghlan,kaskazini mwa Afghanistan. Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani,Frank-Walter Steinmeier amesema,shambulizi hilo ni jeribio la kutaka kuzuia shughuli za ujenzi mpya nchini Afghanistan.Ujerumani ina kiasi ya wanajeshi 3,000 kaskazini mwa Afghanistan,kama sehemu ya vikosi vya amani vya kimataifa.