KABUL: Raia wauawa katika mashambulizi ya NATO
22 Juni 2007Matangazo
Idadi kubwa ya raia wameuawa katika shambulizi lililofanywa na vikosi vya angani vya NATO,dhidi ya wapiganaji wa Taliban,kusini mwa Afghanistan. Kwa mujibu wa polisi wa Afghanistan,shambulio hilo katika wilaya ya Helmand,limeua Wataliban 20 na raia 25-miongoni mwao wakiwepo wanawake 9 na watoto 3.Msemaji wa NATO,amewalaumu wanamgambo wa Taliban kuwa kwa makusudi walivipotosha vikosi vya NATO,kulenga nyumba za wakazi.Nchini Afghanistan,siku hizi za karibuni,lawama zimezidi kuhusika na jinsi vita vinavyoongozwa na vikosi vya NATO na vya Marekani,dhidi ya Wataliban, wakati idadi ya wahanga wa kiraia, ikizidi kuongezeka.