Kabul. Raia 50 wahofiwa kuwa wameuwawa na jeshi la NATO.
27 Oktoba 2006Matangazo
Maafisa wa Afghanistan wamedai kuwa kiasi cha raia 50 wameuwawa katika mashambulizi ya jeshi la NATO kusini mwa nchi hiyo siku ya Jumanne.
Wanakijiji wamesema kuwa mashambulizi ya mabomu yalichukua muda wa saa nne na kwamba nyumba 25 zimeharibiwa katika operesheni hiyo katika wilaya ya Panjwai katika jimbo la Kandahar.
Rais Hamid Karzai amesema ameteua kundi la wachunguzi kuhusiana na madai hayo.
NATO imesema kuwa wapiganaji 48 wameuwawa katika mashambulio hayo lakini pia imekiri kuwa imepata taarifa za kuaminika kuwa raia pia wameuwawa.
Ofisi ya umoja wa mataifa nchini Afghanistan pia imetoa wito wa kufanyika uchunguzi wa kina.