KABUL : Operesheni ya NATO kutokomeza Taliban
5 Septemba 2006Umoja wa Kujihami wa Mataifa ya Magharibi NATO umesema leo hii kwamba shambulio lake kubwa kutokomeza kundi lililofufuka upya la Taliban kusini mwa Afghanistan linawafanya wapiganaji hao wajibanze wakati mapigano makali yakiendelea.
Msemaji wa NATO Quentin Innes amesema wanazidi kuwazingira Taliban na kwamba wamewatia kwenye mtego fulani.
Mwanajeshi mmoja wa Canada aliuwawa na wengine kadhaa kujeruhiwa alfajiri ya jana katika mashambulizi ya bahati mbaya kutoka ndege za Kimarekani wakati operesheni dhidi ya Taliban ikiendelea kusini mwa Afghanistan.
Wiki iliopita NATO ilianzisha Opresheni Medusa ambayo ni operesheni kubwa ya ardhini dhidi ya kundi la Taliban linalozidi kuimarika katika jimbo la Kandahar kitovo kikuu cha kidini kwa kundi hilo la msimamo mkali wa Kiislam.