KABUL: Operesheni kuu ya NATO dhidi ya Wataliban
7 Machi 2007Matangazo
Vikosi vya kimataifa ISAF vinavyolinda amani nchini Afghanistan,vimeanzisha operesheni kubwa dhidi ya Wataliban kusini mwa nchi hiyo.Msemaji wa vikosi hivyo vinavyoongozwa na NATO amesema, hiyo ni operesheni kubwa kabisa kupata kufanywa dhidi ya Wataliban na wafanya biashara wa madawa ya kulevya wanoshirikiana nao.Wanajeshi 4,500 wa NATO na 1,000 wa Afghanistan wanashiriki katika operesheni hiyo ya kijeshi.Vikosi hivyo hasa vinajaribu kuleta usalama katika wilaya ya Helmand ambako kiwanda cha maji kinafanyiwa ukarabati na kupanuliwa.Shirika la NATO,lina jumla ya wanajeshi 33,000 nchini Afghanistan. Wanajeshi wa Ujerumani wapatao kama 3,000 wapo sehemu ya kaskazini yenye utulivu wa aina fulani.