KABUL: Ndege za Ujerumani zawekwa chini ya mamlaka ya NATO
10 Aprili 2007Matangazo
Ndege sita za Ujerumani aina ya tornado zilizowasili nchini Afghanistan wiki iliyopita, zimewekwa nchini ya mamlaka ya shirika la kujihami la kambi ya magharibi, NATO.
Ndege hizo ziko katika kambi ya jeshi la Ujerumani huko Mazar i Sharif na zitatumiwa kupiga picha zitakazotumiwa kulisaidia jeshi la muungano kupanga operesheni zake dhidi ya waasi wa kundi la Taliban.
Shirika la NATO liliziomba ndege hizo kuweza kutafuta maficho ya wanamgambo wa Taliban.
Kwa mujibu wa idhini iliyotolewa na bunge la Ujerumani mwezi uliopita, ndege hizo haziruhusiwi kutumika kwenye mapambano.