1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabul. NATO yadai kutimiza malengo yake Afghanistan.

14 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDCY

Majeshi ya NATO yanasema kuwa yamefanikiwa karibu theluthi mbili ya malengo yake katika mapambano dhidi ya wapiganaji wa Taliban kusini mwa Afghanistan.

Msemaji wa NATO amesema kuwa operesheni hiyo inaweza kuendelea kwa jumla ya wanajeshi waliopo hata kama majenerali wa NATO wameomba wanajeshi zaidi 2,500 kuweka kuharakisha mashambulizi hayo.

NATO tayari inawanajeshi 20,000 nchini Afghanistan .

Wizara ya ulinzi ya Ujerumani imesema siku ya Jumanne kuwa haitatuma wanajeshi kusini mwa Afghanistan , ikisema kuwa wanajeshi 2,900 ambao wamewekwa kaskazini mwa nchi hiyo wanafikisha idadi ya wanajeshi 3,000 ambao ndio kikomo kilichowekwa na bunge.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice ameonya kuwa Afghanistan inaweza kuwa ngome ya magaidi iwapo mataifa ya magharibi kwa mara nyingine tena yataruhusu nchi hiyo kuporomoka.