KABUL: Mwanajeshi wa NATO auwawa
29 Septemba 2006Matangazo
Mwanajeshi mmoja wa shirika la NATO ameuwawa leo katika mripuko uliotokea kwenye mkoa wa Kandahar kusini mwa Afghanstan. Jeshi la NATO halijataja jina la mwanajeshi huyo aliyeuwawa.
Afghanistan inakabilwia na machafuklo mabaya zaidi tangu kuangushwa kwa utawala wa Taliban mnamo mwaka wa 2001.
Shirika la NATO lilikubali jana kuchukua mamlaka ya kulind amani katika maeneo yoe ya Afghanistan kuanzia mwezi ujao baada ya Marekani kuahidi kupeleka wanajeshi elfu 12 zaidi kutoka kwa kambi zake zilizo eneo la mashariki kujiunga na kikosi cha NATO.