KABUL: Majeshi ya NATO na Afghanistan yawaua wanamgambo wa 150 wa Taliban.
11 Januari 2007Matangazo
Majeshi ya NATO pamoja na Afghanistan yamewauwa wanamgambo takriban mia moja na hamsini walioonekana wakati wa usiku wakiingia nchini humo wakitokea Pakistan.
Majeshi ya NATO yametoa taarifa iliyosema wanamgambo hao walionekana mpakani wakiwa na mipango ya kuvishambulia vikosi vya Afghanistan.
Wanamgambo hao waliojigawa katika makundi mawili waliandamwa na kushambuliwa kutoka hewani na pia na majeshi ya nchi kavu katika mpaka, kwenye jimbo la mashariki la Pakistan.