1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL : Kikosi cha NATO lazima kiboreshwe

24 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBop

Kikosi cha Umoja wa Kujihami wa Mataifa ya Magharibi NATO nchini Afghanistan kimesema leo hii Rais Hamid Karzai alikuwa na haki ya kukasirika juu ya mauaji ya raia katika operesheni za kijeshi za umoja huo na kwamba kuna haja ya kuboresha mfumo wa shughuli za kikosi hicho.

Karzai hapo jana amekosowa majeshi ya Umoja wa Kujihami wa Mataifa ya Magharibi yanaongozwa na Marekani kwa operesheni zao holela na matumizi ya nguvu kupia kiasi na bila ya kuratibu shughuli zao hizo na serikali.

Nicholas Lunt msemaji wa kiraia wa kikosi cha Kimataifa cha Usaidizi wa Usalama ISAF kinachongozwa na NATO amesema anahisi Rais Karzai alikuwa mkweli na alikuwa na sababu ya kukasirika na kwa hiyo inabidi waboreshe namna wanavyoendesha operesheni zao.

Hata hivyo amesisitiza kwamba hakuna askari wa ISAF anayekusudia kuuwa raia tafauti na ilivyo kwa Taliban kwamba huwa wanawauwa raia kwa makusudi.