1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabul. Karzai aunda tume kuchunguza madai ya wafungwa kuteswa.

15 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CG1H

Rais wa Afghanistan Hamid Karzai ameteua kamati ya uchunguzi wa madai kuwa wafungwa katika jela za Afghanistan wanateswa. Kundi la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limedai kuwa majeshi yanayoongozwa na NATO ya ISAF yamewaweka wafungwa katika mateso baada ya kuwakabidhi kwa maafisaa wa Afghanistan. Katika mahojiano na televisheni ya DW, kamanda wa jeshi la ISAF kutoka Ujerumani jenerali Egon Ramms amekiri kuwa huenda kuna ukweli katika shutuma hizo.

Ametoa wito kwa maafisa wa Afghanistan kuwatendea vizuri wafungwa kwa mujibu wa mikataba ya haki za binadamu.