KABUL: Karzai atasaidiwa na NATO kuijenga upya nchi
21 Julai 2006Matangazo
Katibu Mkuu wa Shirika la kujihami la nchi za magharibi NATO,Jaap de Hoop Scheffer amemuhakikishia rais Hamid Karzai wa Afghanistan kuwa ataendelea kupata msaada kuijenga upya nchi yake.Vile vile,waasi wa Kitaliban wanapaswa kupigwa vita,alisema de Hoop Scheffer alipokutana na Karzai mjini Kabul.Shirika la NATO hivi sasa limetawanya huduma za vikosi vyake vya kulinda usalama kusini mwa Afghanistan.Idadi ya wanajeshi hao iliyokuwa kama elfu 10 sasa imeimarishwa kufikia elfu 16.