KABUL: Jeshi la NATO lawaua waasi 38 wa Taliban
25 Oktoba 2006Matangazo
Jeshi la NATO nchini Afghanistan limesema limewaua waasi 38 wa Taliban katika mashambulio dhidi ya wanamgambo wanaorudi na kuingia eneo la kusini mwa nchi hiyo, ambalo limekabiliwa na mapigano makali katika siku za hivi karibuni.
Maafisa wa Afghanistan katika wilaya za mkoa wa Kandahar, ngome ya waasi wa Taliban, wamethibitisha kwamba kumekuwa na mashambulio makubwa ya mabomu.