KABUL: Jeshi la NATO lasema waafghanistan 12 waliuwawa kwenye operesheni zake
27 Oktoba 2006Matangazo
Jeshi la NATO limethibitisha kwamba raia takriban 12 waliuwawa kusini mwa Afghanistan mapema wiki hii wakati wa uvamizi wa ngome ya waasi wa Taliban.
Maafisa wa Afghanistan katika eneo hilo wanadai kwamba watu wasiopungua 50 waliuwawa katika operesheni za jeshi la NATO.
Wakaazi wa wilaya ya Panjwai katika jimbo la Kandahar, wanasema mabomu yalivurumishwa kwa muda wa saa nne na nyumba 25 zikaharibiwa kabisa katika mashambulio hayo.
Jeshi la NATO limesema litashirikiana na wizara ya ulinzi ya Afghanistan kuyachunguza madai hayo. Msemaji wa NATO amesema waasi 48 wa kundi la Taliban waliuwawa katika uvamizi wa Jumanne juma hili.
Wakati haya yakiarifiwa watu 14 wameuwawa leo kwenye shambulio la bomu kusini mwa Afghanistan.