1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabul. Hali ni shwari nchini Afghanistan yasema majeshi ya NATO.

23 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFUD

Majeshi ya kulinda amani ya NATO nchini Afghanistan yatawekwa hivi karibuni katika maeneo ya nchi hiyo upande wa magharibi ambako hali inaonekana kuwa shwari zaidi, na huenda pia yakawekwa katika maeneo yenye hali ya wasi wasi upande wa kusini.

Generali James Johns wa majeshi ya Marekani , akiwa pamoja na wabunge kutoka mataifa wanachama wa NATO mjini Kabul, ameieleza hali ya usalama nchini Afghanistan kuwa ni imara, pamoja na kwamba kunatokea mashambulizi ya hapa na pale mara kwa mara.

Wakati Afghanistan inajitayarisha kuingia katika hatua nyingine ya kidemokrasia kwa kufanya uchaguzi wa bunge hapo Septemba 18, Jenerali Johns amesema nchi hiyo bado iko katika hali ya wasi wasi kutokana na uwezekano wa kushambuliwa kwa ghafla, na waasi.