1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabul. Afghanistan yaanza maombolezi baada ya shambulio la bomu.

7 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C79H

Watu nchini Afghanistan wameanza siku tatu za maombolezi , kufuatia shambulio la bomu la kujitoa muhanga kaskazini mwa nchi hiyo ambapo watu kiasi ya 40 wameuwawa na wengine 100 wamejeruhiwa.

Shambulio hilo , ambalo limesababisha vifo vya wabunge sita , lilitokea wakati ujumbe wa ngazi ya juu ulipokuwa ukitembelea kiwanda cha sukari katika jimbo la Baghlan. Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier ameshutumu shambulio hilo, akilieleza kuwa ni jaribio la kuzuwia ujenzi mpya nchini humo.

Steinmeier amesema katika taarifa kuwa kiwanda hicho cha sukari ni moja kati ya miradi kadha ambayo imekuwa ikipatiwa msaada na jeshi la Ujerumani lililoko katika nchi hiyo kama sehemu ya jeshi la kimataifa linalosaidia kurejesha hali ya usalama linaloongozwa na NATO.