1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jurgen kukiongoza kikosi cha mpira wa miguu Korea Kusini

Hawa Bihoga
27 Februari 2023

Jurgen Klinsmann, aliyeshinda Kombe la dunia akiwa mchezaji na kuiongoza Ujerumani kufika nusu fainali kama kocha, ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa Korea Kusini.

https://p.dw.com/p/4O17P
FUSSBALL WM Katar 2022 Pressekonferenz: TSG-Mitglied Jürgen Klinsmann (Deutschland)
Picha: Pressebildagentur ULMER/picture alliance

Shirikisho la mpira wa miguu la Korea Kusini limesema kwamba Jurgen atawasili nchini humo Juma lijalo na mkataba wake utaanza mwezi Machi na utakwisha 2026.

Borussia Moenchengladbach yajizatiti kileleni mwa Bundesliga

Maisha ya soka ya Juegen mwenye rekodi nzuri kama mashambuliaji amechezea Inter Milan, Tottenham na  Bayern Munich. Amefunga mabao 47 katika mechi 108 alizoichezea Ujerumani.

Kadhalika aliiongoza Ujerumani hadi nafasi ya tatu katika Kombe la Dunia la 2006 katika ardhi ya nyumbani, kabla ya kuchukua mikoba ya Bayern na kisha Marekani.