Jukwaa la Maendeleo kwa Afrika laasisiwa Berlin
25 Aprili 2007Kulisaidia zaidi bara la Afrika ndio shabaha iliowekwa na serikali ya Ujerumani, ikiwa ni mwenyekiti wakati huu wa kundi la dola kuu 8 tajiri ulimwenguni (G-8).Juhudi mpya kuelekea shabaha hiyo ikipangwa kuchukuliwa, basi vigogo mashuhuri viliojiweka usoni havikuwa na kwengineko kwa kuelekea kwa kikao chao bali Berlin.Kikundi hiki kimejiita “JUKWAA LA KUTETEA MAENDELEO YA AFRIKA “.
Jukwaa la maendeleo ya Afrika –“Africa Progreess Panel” linajumuisha watu mashuhuri kama Katibu mkuu wa zamani wa UM Kofi Annan, mshindi wa hivi punde wa Zawadi ya Nobel kwa amani Muhammad Yunus kutoka Bangladesh,Robert Robin, waziri wa fedha wa Marekani katika utawala wa Bill Clinton, na Michel Camdessus,mkurugenzi wa zamani wa Shirika la Fedha Ulimwenguni (IMF).
Kofi Annan haliangalii jukwa hii kuwa mojawapo ya mashirika kadhaa yalioundwa juu ya bara la Afrika:
“Jukwaa hili litajishughulisha hasa na vitendo .Hatutakua kundi jengine linalotoa ripoti tu.Tutachoweka mezani, ni maarifa makubwa na maamuzi ambayo tungependa kuagawana na viongozi kwenye mikutano ya uso kwa uso pamoja nao na taarifa tutakazozitangaza hadharani ili kuzitaka serikali kutilia mkazo upya juhudi zao ili kutimiza shabaha zinazolengwa kufikiwa.”
Shabaha za mkutano wa kilele wa Millennium wa UM ambaozo ni kupunguza umasikini kwa nusu hadi ifikapo 2015,kwa bara la afrika shabaha hii haitaweza tena kufikiwa ikiwa nchi za kundi la dola 8 tajiri linalojumuisha pia Russia,hazitatimiza haraka ahadi zao zilizotoa tangu 2002 katika mkutano wao wa kilele huko Gleneagles,Scotland.
Kofi Annan akazizindua dola hizo kwamba hazitakuwa na hisia nzuri juu ya Afrika ikiwa haizikutimza ahadi zao.Alisema,
“Kwanza, serikali za nchi za kiafrika ndizo zenye jukumu kubwa,lakini zinahitaji msaada.Na msaada huo umeahidiwa kutolewa na natumai, matumaini hayo yatatimizwa.”
Bado dola zote kuu 8 za kundi la G-8, ziko mbali sana kutimiza ahadi zilizoweka .Hata Ujerumani haikutimiza ahadi zake,anasema Bob Geldorf,mwanamuziki wa rock,aliegongwa vichwa vya habari duniani kote kwa burdani alioandaa “LIVE-AID’ kulisaidia bara la Afrika pia mwanachama wa jukwaa hili la maendeleo ya Afrika.
“ Pale matajiri wanapotoa ahadi kwa masikini,hii ni ahadi kubwa kabisa mtu anayotoa.Kwasababu kuivunja ahadi hiyo,unaua binadamu.”
Asema Bob Geldorf, akiongeza kusema kwamba, ukiwajumuisha pamoja watu wenye busara,wanowaza na kufikiri,watu wanaoizingiatia hali ya ulimwengu ilivyo,wanafalsafa,wasomi,hii si maandamano ya malalamiko-hii ni kukaa na kuwaza la kutenda.
Ni kuwaza basi kwa dola kuu 8 tajiri katika sayari hii ili kutimiza jukumu lao ulimwenguni.