1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jukwaa juu ya hali ya hewa Potsdam

9 Oktoba 2007

Jukwaa juu ya badiliko la hali ya hewa likiwajumuisha washindi wa zawadi ya Nobel 15 umefunguliwa Berlin.

https://p.dw.com/p/C7s1

Kanzela Angela Merkel wa Ujerumani, anakutana leo mjini Potsdam,nje ya Berlin,na wataalamu mashuri wa taftishi za kisayansi ili kupanga pamoja nao mkakati wa kupambana na dhara zinazosababisha mabadiliko la hali ya hewa.Bibi merkel anashauriana na washindi 15 wa tuzo la Nobel pamoja na wataalamu 30 taftishi za kisayansi wa kimataifa pamoja na wanasiasa na watu maarufu katika jamii.

Shabaha ya kikao cha ni kuzingatia jinsi gani mabadiliko ya hali ya hewa yaweza kudhibitiwa.

Ilioandaa hasa kikao hiki ni Taasisi ya Potsdam juu ya zaftishi za hali ya hewa iliopo Potsdam, si mbali na jiji kuu Berlin.Taasisi hii tangu 1992 imekua ikijishughulisha na jinsi sayari yetu inavyoathirika.

Nyuzi 15 Celsius ni kipimo kisicho cha kawaida kwa adhuhuri mnamo mwezi wa Januari.Katika Taasisi ya taftishi za hali ya hewa mjini Potsdam ,anahudhuria wakati huu kikao hicho waziri wa mazingira wa Ujerumani Bw.Sigmar Gabriel.

Kabla kuwasili kwake katika jukwaa hilo,macho ya waandishi habari,wanakamera za TV yalikodolewa Bw.Hans Joachim Schellnhuber,mkurugenzi wa Taasisi hiyo ya Potsdam:

“Najua mimi sitakuwa tena wa kushughulikiwa,lakini hadi atakapowasiliBw.Sigmar Gabriel-waziri wa mazingira wa Ujerumani) ninajaza pengo lake.”

Alisema mkurungenzi wa taasisi hiyo.

Bw.Schellenhüber anauelewa vyema mchezo unavyoenda na anacheza nay eye.Bila ya taabu anatoa habari na anajibu maswali kama vile kuwa na majira ya baridi-winter ilhali sio baridi sana kuna mafungamano na badiliko la hali ya hewa ?

Jibu lake:

“Chini ya misingi ya kisayansi,ningesema hicho ndicho chanzo chake.Nasema kwamba ,unapoupanda mlima mkubwa,basi unajua takriban wakati mwingi unapanda tu kama ilivyo katika vipimo vya hali ya hewa.

Halafu unafikia sehemu zisizo na mabonde kwenye mlima huo na hapo unashuka kidogo….Nasema kwa ufupi, badiliko la hali ya hewa ni vigumu hivi sasa kubashiri.”

Risala anayoitoa Bw.Schellnhuber na kufungamanisha na nyengine ni kuwa sio imechelewa kabisa kuchukua hatua madhubuti kuzuwia kuzidi kuchafuka kwa hali ya hewa.Akitoa risala hii lakini, hapendi kujiingiza katika mabishano ya kisiasa bali hiyo ni nasaha yake tu anayoitoa.

Lakini kiwa kama ilivyo leo huko Potsdam washindi 15 wa zawadi ya Nobel wamejumuika pamoja na wakitoka fani mbali mbali,basi hiyo pia ni ishara ya kisiasa wanayotoa.

Imepangwa kujadiliana katika duru ndogo lakini kwa upeo wa hali ya juu kabisa-jinsi gani sayari yetu hii inaweza kuendeshwa.Kuvileta pamoja vichwa vya werevu na wataalamu kutoka kila pembe ya dunia mjini Potsdam, kuona kidogo mila za Sanssouci ndio lengu lao-asema mkurugenzi wa Taasisi.

Mwishoni mwa kikao hiki inatarajiwa kutolewa kumbukumbu kwa jina la ‘POTSDAM MEMORANDUM’ .kumbukumbu hiyo itaodhoresha hatua mbali mbali zinazopaswa kuchukuliwa kupiga vita mabadiliko ya hali ya hewa.

Mkutano juu ya hali ya hewa kisiwani Bali, Indonesia hapo desemba mwaka huu,ndio anaoutupia macho Bw.Schellnhuber.Anafikiri mbali,kwani asema hakuna njia nyengine isipokua hiyo.