1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Juhudi za kutafuta amani ya Somalia zaendelea

Siraj Kalyango5 Desemba 2007

Je! Rais Yusuf yu mahtuti?

https://p.dw.com/p/CXMW
Raia moja wa kisomali akiwa nje ya magofu ya majengo yaliyobomolewa na vita vya wenyewe kwa wenyewe mjini MogadishuPicha: AP

Serikali ya Somalia imekubali umoja wa Mataifa pamoja na mashirika yake ya kimisaada kurejelea tena shughuli za utoaji misaada katika eneo la kusini magharaibi mwa nchi hiyo.Serikali ya Mogadishu ilikuwa imeamuru viwanja vya ndege pamoja na bandari katika eneo la Lower Shebelle kutotumiwa na mashirika ya kimisaada ya kimataifa pamoja na ya umoja wa Taifa iliokuwa ikitoa msaada kama vile chakula kwa watuwa eneo hilo.

Matokeo mbalimbali yanatokea karibu kwa wakati mmoja kuhusu Somalia, nchi ambayo imekumbwa na mapigano ya ya kiukoo kwa mda mrefu.

Utawala wa Mogadishu,jana ulikuwa umeamuru mashirika yote ya kimisaada yasitishe kazi zake katika eneo la kusini magharibi mwa nchi hiyo.

Hatua hiyo ilipingwa na shirika la mpango wa chakula duniani WHO ambalo limekuwa likitumia uwanja wa ndege pamoja na bandari kutoa msaada wa chakula kwa maelfu ya wakimbizi wa kisomali ambao wameutoroka mji mkuu wa Somalia –Mogadishu- kutokana na vita.

Mohammed Hurre ni mkuu wa juhudi za kuiletea amani nchi ya Somalia, aelezea hali ilivyo kwa sasa katika mji wa Mogadishu,

‚...Mogadishu baado nikama msitu ambapo kila mtu anafanya kile atakacho.Wapiganaji wa chini kwa chini baado wapo wakiwa na silaha zao, na siku chache zilizopita walishambulia magari mawili ya kijeshi na kuwauwa maafisa wawili wa kijeshi.Hali kama hii itaendelea na serikali inajaribu kadri ya uwezo wake.’ amesema Hurre.

Wapiganaji wa umoja wa kiislamu wanaoupinga utawala wa sasa wa Mogadishu wakiwa wanazidisha hujuma zao wamekataa mwito wa kufanya mazungumzo na utawala uliowatimua madarakani ukisaidiwa na majeshi ya Ethiopia.Sheikh Sharif Ahmed, mwenyekiti wa muungano wa makundi ya ukombozi wa Somalia-ARS, ambae kwa sasa yuko nchini Eritrea, ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa mazungumzo yanaweza tu kufikiriwa ikiwa Ethiopia imeoandoa majeshi yake kutoka ardhi ya Somalia.

Yeye waziri wa mashauri ya kigemnni wa Marekani Bi Condoleezza Rice yuko katika eneo hilo la 'upembe wa Afrika' , miongoni mwa mengine atayojadilia na viongozi wa eneo hilo ni mgogoro wa Somalia.

Hata hivyo rais Abdullahi Yusuf huenda asihudhurie.

Hii nikutokana na kuwa yuko Nairobi nchini Kenya ambako amelazwa.Duru fulani zinasema kuwa hali yake ya kiafya si nzuri.Lakini mjumbe mmoja amesema kuwa kuja kwake katika hospitali ni sababu za uchunguzi tu wa kawaida wa afya yake.

Balozi wa Somalia nchini Kenya, Mohammed Ali Nur,ambae anasema rais mwenye umri wa miaka 72,ingwa wengine wanasema umri wake hasa ni miaka 80, hali yake ni sawa na wala sio ile inayosemwa na baadhi ya vyombo vya habari.

Hata hivyo haijulikani ikiwa wapinzani wa utwala wa sasa wa Mogadishu watahusishwa katika mkutano wa Addis Ababa.Aidha Bi Condeleezza Rice anatarajiwa kuuhimiza utwala wa Mogadishu kuuhusisha upinzani katika maamuzi ya nchi hiyo ili kukomesha mgogoro ambao umeendelea kwa mda mrefu.