1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JUBA:Serikali ya Uganda yakataa mapendekezo ya LRA

20 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG5r

Serikali ya Uganda imekataa mapendekezo ya kundi la waasi wa Lords Resistance Army LRA katika mazungumzo yanayofanyika Juba nchini Sudan.

Mapendekezo hayo ya LRA ni pamoja na kuvunjwa kwa jeshi la taifa na kulipwa waasi hao fidia kwa madai kwamba walifanyiwa ukatili.

Naibu waziri wa mambo ya nje wa UgandaOkello Oryem amesema serikali ya Uganda inakubaliana na mwito wa kusitisha mapigano lakini jambo hilo linaweza kufanyika baada ya kumalizika mazungumzo ya amani ya Juba.

Msemaji wa ujumbe wa LRA Obonyo Olweny amesema msimamo huo wa serikali ya Uganda unazusha shaka kama kweli serikali hiyo ina nia ya kutaka amani.