1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JUBA : Waasi wa LRA waanza kukusanyika kwenye vituo 2

11 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDDP

Mamia ya waasi wa Uganda akiwemo naibu kamanda wao wamekusanyika katika sehemu mbili ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya suluhu yaliotiwa saini kati yao na serikali wiki tatu zilizopita.

Iwapo habari hizo zitathibitishwa kuwepo kwa naibu kamanda wa kundi la LRA Vincent Otti itakuwa imarisho kuu la juhudi za kukomesha mojawapo ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Afrika vilivyodumu kwa muda mrefu na vya kikatili kabisa.

Makamo wa Rais wa Sudan ya Kusini Riek Machar amewaambia waandishi wa habari kwamba waasi hao wamejitokeza katika kituo walichotakiwa wakusanyike cha magharibi huko Ri-Kwangba na pia wamejitokeza huko Owiny-ki-Bul.

Pia amesema na hata Joseph Kony hayuko mbali.