Joto lahusishwa na vifo vya watu 3,100 Ujeumani
30 Septemba 2023Matangazo
Watafiti wa afya wa taasisi ya Robert Koch (RKI) ya Ujerumani wamesema kwa mwaka huu pekee takriban watu 3,100 wamekufa nchini Ujerumani kutokana na joto kali.Idadi kubwa ya waliopoteza maisha ni wa umri miaka 75 au zaidi. Utafiti unaonesha, wanawake hufa zaidi kuliko wanaume kutokana na joto, kwa kuwa kuna na idadi kubwa ya wanawake miongoni mwa wazee.Rekodi za taasisi RKI zinaonesha vifo vinavyohusiana na joto nchini Ujerumani kufikia watu 6,000 katika miaka ya 2018, 2019 na 2015. Lakini katika miaka ya 2014, 2016, 2017 na 2021, kulikuwa na vifo kati ya 1,000 na 1,700.