Joto la kiasa linaendelea kughubika Warepublican
4 Februari 2021Leo Alhamisi bunge linatarajiwa kupiga kura muhimu ya kisiasa, ambayo itaamua ikiwa Mrepublican huyo wa jimbo la Georgia ataondolewa majukumu yake ya kamati, na kuongeza wasiwasi juu ya mbinu gani bora ya kisiasa itakayoweza kutatua mvutano ulioibuka katika chama cha Republican tangu Donald Trump aliposhindwa katika uchaguzi mkuu.
Wademokrat mapema wiki hii, walitoa muda wa mwisho kwa Warepublican kumvua Greene majukumu yake ya kamati na iwapo watashindwa basi watamvua wao wenyewe. Shinikizo la pande mbili liliibuka baada kiongozi wa wachache katika bunge la Seneti Mitch McConnell kumuita Greene "Muongo " na "saratani" kwa chama. Soma Ziadi Mvutano kati ya rais Trump na wademocrat unaendelea
Lakini kiongozi wa wachache katika baraza la wawakilishi Kevin McCarthy, siku ya Jumatano aliondoa uwezekano kuchukua hatua zozote dhidi ya Greene. Badala yake, aliwashutumu Wademokrat kwa "unyakuaji madaraka wa kichama" kwa kumlenga Greene, ambaye wakati mmoja alisema kampuni ya kifedha ya Kiyahudi huenda ilishiriki katika njama ya kusababisga moto wa msitu jimboni California kwa kutumia miale ya angani.
Azma ya kumvua madaraka Greene
Mwenyekiti wa kamati ya kanuni za bunge Jim McGovern, amesema wanaazimia kumvua Greene wadhifa wake. Uamuzi wa McCarthy kumuunga mkono Greene unakuja wakati chama hicho kina mgawanyiko wa kifikra baada ya kushindwa kwa Trump.
Siku ya Jumatano, Wabunge wa Republican walizuia juhudi za wahafidhina kumng'oa Mwanachama wa Republican mwakilishi Liz Cheney kutoka jukumu lake la uongozi. Cheney, mtoto wa Makamu wa rais wa zamani Dick Cheney, alikuwa amewakasirisha wafuasi wa Trump kwa kupiga kura ya kumshtaki juu ya ghasia zilizoshudiwa katika majengo ya Bunge. Soma Zaidi Wademocrat watoa wito rasmi ili Trump aondolewe madarakani
Greene ameonyesha kuunga mkono wito wa vurugu dhidi ya Wademokrat, na taarifa za uwongo juu ya ufyatuaji risasi shuleni na nadharia kuwa Wademoktrat wanaendekeza unyanyasaji dhidi ya watoto.
Matamshi ya Greene
Nadharia za njama ambazo amekumbatia ziliibuka wakati wa mkutano wa kamati ya wabunge wa Republican siku Jumatano, Baadhi ya waliohudhuria walisema Greene aliomba msamaha kwa wenzake, ingawa kulikuwepo na wanaopingana na matamshi hasa aliyotoa.
Kinyume na taarifa hiyo, wiki za hivi karibuni kupitia mtandao wake wa Twitter, Greene ameapa kuwa hatarudi nyuma au kuomba msamaha na aliwataja wakosoaji wake kuwa wasaliti, wanaotumia shinikizo la wademokrat kumwadhibu kuhusiana na juhudi zake za kutafuta pesa kwa ajili ya kampeni yake.
/Afpe