1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JOHANNESBURG : Yagoma kuwapa ukimbizi Zimbabwe

13 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBZt

Afrika Kusini hapo jana imekataa wito wa kuanzisha kambi ya maelfu ya wakimbizi wenye njaa wa Zimbabwe nchini humo ambao kila siku hukimbilia nchini humo kwa kusema kwamba wakifanya hivyo watakuwa wanakiuka taratibu za Umoja wa Mataifa.

Waziri wa mambo ya ndani Nosiviwe Mapisa- Nquakula amesema Afrika Kusini imetia saini mikataba mingi ya Umoja wa Mataifa na kwamba hawataki kuwapa hadhi ya wakimbizi watu wasiotaka kuwa wakimbizi.

Amewaelezea Wazimbawe wengi wanaoingia nchini humo kinyume na sheria kuwa ni wahamiaji wa kiuchumi ambao hawana nia ya kuloweya bali wanachotaka ni kununuwa chakula tu.

Kuna uhaba mkubwa sana wa bidhaa nchini Zimbabwe kufuatia kusambaratika kwa uchumi wa nchi hiyo na msako wa kudhibiti bei na inakadiriwa kwamba Wazimbabwe 3,000 hadi 5,000 huvuka mpaka na kuingia nchini Afrika Kusini kila siku.