1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JOHANNESBURG : Mamluki waachiliwa Zimbabwe

15 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFDQ

Kundi la wanaotuhumiwa kuwa mamluki 62 waliokuwa gerezani nchini Zimbabwe wameachiliwa huru na kurudi Afrika Kusini.

Marge Pain ambaye mume wake Ken alikuwa ni mmojawapo wa watu 70 waliokamatwa mwezi wa Machi mwaka jana wakati ndege yao ilipotua kwenye uwanja wa ndege wa Harare kuchukuwa silaha amesema watu hao wamewasili Afrika Kusini na maafisa wa serikali wako mbioni kushughulikia nyaraka zao.

Serikali ya Zimbabwe ilidai kwamba silaha hizo zilikuwa zimepangwa kutumiwa kumpinduwa Rais Teodoro Obian Nguema kiongozi wa taifa lenye utajiri wa mafuta la Equatorial Guinea.