Johannesburg. Kuvunjwa kwa mabanda poromoka, haki za binadamu zimekiukwa.
10 Septemba 2005Makundi ya haki za binadamu nchini Zimbabwe yamesema leo kuwa hatua ya kuwaondoa wakaazi kadha wa vibanda poromoka mijini imekwenda kinyume na haki ya mamia kwa maelfu ya watu na kuharibu mwenendo wa matibabu ya ukimwi nchini humo, na kutishia mlipuko mwingine wa ugonjwa huo .
Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights watch limemtaka katibu mkuu wa umoja wa mataifa Kofi Annan kuchunguza kampeni hiyo na kumshutumu rais Robert Mugabe na serikali yake kwa kuzuwia juhudi za umoja wa mataifa za kuwasaidi wahanga.
Pia shirika hilo la haki za binadamu limesema kuwa wale waliohusika na kupanga na kutekeleza zoezi hilo lazima wafikishwe mbele ya sheria.