JOHANNESBERG: Tony Blair ziarani Afrika Kusini
31 Mei 2007Matangazo
Waziri Mkuu wa Uingereza anayeondoka madarakani, Tony Blair, amewasili Afrika Kusini akiwa katika ziara yake barani Afrika.
Katika ziara yake ya siku mbili nchini humo, Tony Blair anatarajiwa kukutana na Rais Thabo Mbeki na aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Mzee Nelson Mandela.
Tony Blair anatarajiwa kutoa hotuba yake ya mwisho kama waziri mkuu wa Uingereza katika Chuo Kikuu cha Afrika Kusini mjini Johannesburg.
Hotuba hiyo itagusia mizozo ya Zimbabwe na Darfur, biashara ya kimataifa na pia mkutano wa juma lijalo wa mataifa manane yaliyostawi kiviwanda, G8, nchini Ujerumani.
Tony Blair tayari amezitembelea Libya na Sierra Leone na anatarajiwa kuachia madaraka tarehe ishirini na saba mwezi huu.