Joachim Sauer mume wa kansela Merkel
14 Septemba 2017Ni mara chache ameonekan, huyo ndio Merkel na hata mume wake Joachim Sauer yuko karibu hivyo hivyo si mtu wakujitokeza mara nyingi mbele za watu.a pamoja na mkewe Merkel katika tamasha la muziki wa Opera mjini Bayreuth. Kuhusu masuala ya kisiasa hasemi lolote.
Kujitokeza mbele ya vyombo vya habari , kama wanavyofanya baadhi ya wake za marais wa Marekani, hilo kwa Joachim Sauer halipo kabisa. Na hata ukimlinganisha na mwenza wa kansela wa zamani Doris Schoeder-Kopf ama Hannelore Kohl, Sauer ni tofauti kabisa. Mahojiano na waandishi wa habari hayapendelei kabisa. Sio kwamba ni mwenye haya, la hasha, hapendelei tu kumfunika mke wake Angela Merkel. Kama hil halitoshi, mtu huyo ambaye ni sehemu ya Kansela wa Ujerumani ni mtaalamu mkubwa wa masuala ya kemia, ambaye amekwisha pewa tuzo kadhaa.
Profesa Dr. Sauer alianza kufanyakazi zake mwaka 1967 akifanya utafiti wa kemia katika chuo kikuu cha mjini Berlin cha Humboldt. Katika iliyokuwa Ujerumani mashariki DDR, alikuwa mmoja kati ya wanasayansi wanaoaminiwa kimataifa, ambao hawakuwa wanajihusisha na kitengo cha ujasusi cha Ujerumani mashariki. Baada ya kufanyakazi katika sehemu mbali mbali anaongoza tena leo hii kikundi cha utafiti wa kemia ya vyakula katika chuo kikuu cha Humboldt , kikifanya utafiti juu ya tathmini ya vyakula mbali mbali na utafiti wa kinadharia kuhusu maumbo, nishati na mchakato wa mwili kuweza kuchakachua chakula.
Tuzo ya Nobel
Kama uvumi uliotokea mwaka 2015, kwamba kuhusiana na hatua za Angela Merkel kufungua mipango ya nchi hii kwa wakimbizi na wahamiaji, kumekuwa na matamshi katika duru za wataalamu, kwamba mume wake Joachim Sauer anaweza kupata tuzo ya Nobel ya kemia. Barack Obama alimuita wakati walipokutana na Merkel kwa kiasi kikubwa kwa jina la Profesa tu.
Sauer alimfahamu Merkel katika miaka ya 1980 wakati wakiwa katika chuo cha sayansi mjini Berlin. Walioana mwaka 1989, ikiwa wote ni ndoa ya pili. Katika ndo ya kwanza Sauer ana watoto wawili wa kiume. Kwa upande wa Joachim Sauer kama mtu wa kawaida hilo halijulikani. Kwa upande wa mume wake kile anachosema Merkel, ni kwamba hawazungumzi sana kuhusu siasa, lakini pia ni mshauri mzuri kwa upande mwingine. Wawili hao wanaunganishwa na mapenzi makubwa ya muziki wa Opera na uasili, kwa miaka kadhaa wamekuwa wakifanya safari katika majira ya joto kwenda Tirol ya kusini kutembea.
Mwandishi: Ines Eisele / ZR / Sekione Kitojo
Mhariri: Iddi Ssessanga