Joachim Löw kabla ya kutawaza
30 Mei 2018Anapaswa kulielewa. Amekuwa akiifanya kazi hiyo kwa muda wa miaka kumi na mbili sasa, takriban sawa na alivyo Angela Merkel kama Kansela wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani. Jogi kama anavyoitwa kwa mkato akiwa na fulana yake iliokatwa alama ya V shingoni na anayezungumza Kijerumani kwa lafdhi ya Kusini mwa Ujerumani , ameshika wadhifa wa kocha wa timu ya taifa ya Kandanda, kwa kisiasi ambacho Mjerumani hakumbuki mtu mwengine-hakuna mashindano ya kandanda bila ya yeye kuwepo. Hivi sasa amerefusha mkataba wake na Chama cha kandanda cha Ujerumani (DFB) safari hii hadi 2022, yatakapofanyika mashindano mengine ya Kombe la dunia baada ya 2018.
Kwanini anafanya hivyo wakati yeye ni bingwa mtetezi aliyekwisha tunzwa medali ya juu ya Ujerumani ya utumishi uliotukuka na mtu aliyekwisha chaguliwa Kocha wa mwaka wa Shirikisho la Kandanda la Kimataifa –FIFA na hata uwanja wa michezo wa kwao anakotoka kupewa jina lake ? wakati hayo yakimpa motisha kusonga mbele, kwa hakika hana cha kupoteza.
Kubwa muhimu Katika Timu:
"Kombe la Dunia 2014 yalikuwa mafanikio ya juu kabisa kwetu sote lakini sio mwisho,” anasema Löw mwenye umri wa miaka 58. Ushindi mmoja hautoshi anataka kukamilisha kile ambacho hakijawahi kutimizwa na kocha mwengine wa timu ya taifa kabla yake na ambacho hadi sasa ni mataifa mawili tu yameweza kukifanya Itali(1938) na Brazil (1962) . Kuutetea ubingwa wa kombe la dunia na kulinyakua tena. Katika mahojiano na DW, Löw amesema " Kuendelea kuwa katika kiwango hicho cha juu, kunahitaji jitihada kubwa”.
Bila shaka unaposherehekea mafanikio mengi, ni dhahir unafika mahali shauku inapotea ni jambo la kibinaadamu. Kwa hiyo ni muhimu kuhakikisha unafikia kiwango cha juu bila ya kuporomoka. Löw ana imani na timu yake ambayo pia imekuwa na ujuzi mkubwa, jambo ambalo lilikuwa nadra kwa timu ya Ujerumani hapo kabla. " Bado naona uwezo mkubwa ndani ya timu hii na bado nina hamu kubwa ya kuendelea kufanya kazi na kikosi hiki cha wachezaji, nikiwaendeleza zaidi”.
Mbali na hayo, Löw anajuwa kujivunia kuwa kocha wa timu ya taifa asiyepingika na hujiepusha na shinikizo, jambo ambalo huwakumba makocha wengine wanapofanya juhudi za kutafuta mafanikio. Anaweza kufanya kazi kwa utulivu kabla ya Kombe la Ulaya na Kombe la dunia na bila ya shinikizo kutoka juu. Hayo humsaidia kufikiria jinsi ya kujipanga kwa muda wa wastani au muda mrefu kwa mikakati yake mwenyewe,fikra,falsafa ya mchezo na mbinu za mchezo, pamoja na maendeleo mapya ya kandanda na uchambuzi .
Shauku ya ushindi
Löw anasema ,” huenda tukawa na kitu ambacho wengine watakiona cha kiwenda wazimu katika kombe la dunia nchini Urusi, lakini ni katika kutafuta mbinu mpya na ndiyo maana tunazingatia sana mustakbali wetu ". Anasema hata mashabiki wa Ujerumani huwa na shauku kwa sababu kiwango katika mechi nne zilizopita , dhidi ya England, Ufaransa, Uhispania na Brazil hakikuwa cha kuvutia. Hao wote ni washiriki wakubwa katika Kombe la dunia. Tulitoka sare mara tatu na kupoteza mechi moja, lakini hupaswi kuanza kuwa na wasiwasi anasisitiza kocha Löw.
Löw amekuwa akijiandaa vilivyo kwa matayarisho ya Kombe la Dunia tangu kiasi miaka miwili iliopita. Mwenyewe anasema bila ya mipango hakuna mafanikio, lakini ukiwa na akili iliotulia unaweza kupiga hatua kubwa mbele. Anamaliza kwa kusema, pamoja na yote mashabiki wa kandanda wa Ujerumani wanapaswa kuwa na matumaini na wakati huo huo na tahadhari kwani kuna wakati ambapo mafanikio huwa ni suala la bahati.
Mwandishi: Mohammed Abdul-Rahman/Wiertz,Sarah ( DW Sport)
Mhariri: Grace Patricia Kabogo