Mwanaadamu anavyojimaliza kwa kuvamia vyanzo vya maji
Bernard Maranga15 Januari 2016
Shughuli za wanaadamu kujitafutia riziki zao mara kadhaa huvuuka mipaka ya kimazingira na kutiribua mfumo wa mtegemeano wa viumbe na mazingira yao, na matokeo yake ni kujiharibia maisha yao na viumbe vinavyotegemea mazingira hayo. Hicho ndicho kinachotokea hasa pale wanaadamu wanapovamia vyanzo vya maji kama vile maziwa, mito na chemuchemu.