1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jinping azungumza na Bin Salman

28 Machi 2023

Rais wa China Xi Jinping amefanya mazungumzo kwa njia ya simu leo na mrithi wa kiti cha mfalme nchini Saudi Arabia, Mohammed Bin Salman akipongeza alichokiita hatua ya kupunguzwa mvutano katika Mashariki ya Kati.

https://p.dw.com/p/4PMyU
China | Nationaler Volkskongress
Picha: Mark R. Cristino/REUTERS

Rais wa China Xi Jinping amefanya mazungumzo kwa njia ya simu leo na mrithi wa kiti cha mfalme nchini Saudi Arabia, Mohammed Bin Salman na miongoni mwa yaliyojitokeza ni kiongozi huyo wa China kusifu kile alichokiita hatua ya kupunguzwa mvutano katika Mashariki ya Kati.  

Soma zaidi: Saudi Arabia kuanzisha mahusiano upya na Syria

Katika kauli yake ya kwanza aliyoitowa hadharani, tangu Saudi Arabia na Iran kufikia makubaliano ya amani, rais huyo wa China amesema mazungumzo yaliyoungwa mkono na nchi yake yatabeba dhima kubwa kuimarisha mshikamano wa kanda hiyo na ushirikiano. 

Soma zaidi: Rais wa Iran kumtembelea Mfalme wa Saudi Arabia katika jitihada za kuimarisha mahusiano

Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la Saudi Arabia, Mohammed Bin Salman  amepongeza juhudi za China za kuunga mkono jitihada za  kuyajenga mahusiano ya ujirani kati ya pande hizo mbili.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW