1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jimbo la Rakhine la Myanmar huenda likakabiliwa na njaa kali

8 Novemba 2024

Jimbo la Rakhine nchini Myanmar, ambalo ni makazi ya jamii ya walio wachache ya Warohingya huenda likakabiliwa na njaa kali katika siku za hivi karibuni.

https://p.dw.com/p/4mmy2
Paa la nyumba lililoharibiwa na mabomu huko Rakhine
Paa la nyumba lililoharibiwa na mabomu huko RakhinePicha: Mohammad Jihad/AP/picture alliance

Jimbo la Rakhine nchini Myanmar, ambalo ni makazi ya jamii ya walio wachache ya Warohingya huenda likakabiliwa na njaa kali katika siku za hivi karibuni. Haya ni kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa jana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP kwa jina Rakhine: Njaa inayokaribia.

Ripoti hiyo imesema utabiri unaonyesha kuwa uzalishaji wa chakula wa ndani utakidhi tu asilimia 20 ya mahitaji yake kufikia Machi-Aprili 2025.Mtalaamu wa UN yaonya kuhusu mauaji ya kiwango cha kimbari Myanmar

Pia imeelezea kuhusu msururu wa matukio yanayoingiliana ikiwa ni pamoja na vikwazo kwa bidhaa kutoka kwingineko Myanmar na taifa jirani la Bangladesh, ukosefu wa mapato kwa wakazi, mfumuko mkubwa wa bei, kupungua kwa kiasi kikubwa cha uzalishaji wa chakula, na ukosefu wa huduma muhimu za kijamii.

Kutokana na hayo, UNDP imesema, jamii hiyo ambayo tayari iko katika hatari kubwa inaweza kuwa kwenye ukingo wa kusambaratika zaidi katika miezi ijayo.