Jeshi Tunisia lawafunga wabunge wawili
22 Septemba 2021Hukumu hiyo imetolewa wakati ambapo wasiwasi kuhusu suala la haki za biandamu unaongezeka, baada ya rais kuchukua mamlaka yote mwezi Julai.
Mahakama hiyo imewafungwa Nidal Saudi na Saif Eddine Makhlouf, kiongozi wa chama cha Karama na mkosoaji wa mara kwa mara wa Rais Kais Saied bungeni.
Hukumu hiyo inaifanya idadi ya wabunge waliofungwa kufikia watano.
Taarifa iliyotolewa na mahakama ya kijeshi imesema jaji huyo aliamuru Makhlouf afungwe kwa sababu alitoa kitisho kwa jaji wa kijeshi na kuwahutumu majaji wa kijeshi kwa kuhusika katika kile Makhlouf alichokieleza kama mapinduzi.
Rais Saied alimfuta kazi waziri mkuu, alilisimamisha bunge na kuchukua madaraka kamili Julai 25, hali inayozusha wasiwasi kuhusu nia yake.
Makundi ya haki za binaadamu yameshinikiza kuachiwa kwa mbunge mwingine, Yassin Ayari na yamekosoa matumizi ya mahakama za kijeshi kusikiliza kesi za raia.