Jeshi la Ujerumani Afghanistan
4 Septemba 2008Uchambuzi wa wahariri wa magazeti ya Ujerumani umetuwama zaidi juu ya mada mbili:
Kwanza juu ya harakati za Jeshi la Ujerumani "Bundeswehr" nchini Afghanistan na pili juu ya msukosuko katika uongozi wa chama-tawala cha Social Democratic party (SPD).
Tukianza na gazeti la NEUE OSNABRńCKER ZEITUNG linalochambua nia ya waziri wa ulinzi wa Ujerumani Bw.Jung laandika:
"Anataka kusafisha mikono ya serikali ya Ujerumani kutosema kifuate nini sasa huko Afghanistan:Je, hatua kali zaidi,mapambano zaidi na watalibani ? Au Ujerumani ipeleke huko wanajeshi zaidi ambao hawataleta matokeo yoyote ya maana?Au kifuate nini ?
Bw.Jung hasaidii kitu kwa mbinu hizo anazotumia.
Ukweli ni kuwa ikiwa Bw. Jung binafsi hahoji harakati za jeshi la Ujerumani kila asubuhi anaponyoa ndevu zake,basi hafai kuwa waziri wa ulinzi."
Hayo ni maoni ya Osnabrżcker Zeitung.
Ama gazeti la Mittelbayerische Zeitung laandika kwamba, wajerumani sasa wamegeuka shabaha kubwa ya kuhujumiwa na hakuna aliejiandaa kuikabili hali hii.Sababu ni kuwa :
"Kushiriki kwa majeshi ya Ujerumani katika vita nchini Afghanistan kulipambwa uzuri kusibainishe hatari zake.Serikali sasa iwakomboe raia na wanajeshi na ijitwike jukumu la makosa yake.Jeshi la Ujerumani linabidi sasa kujirekebisha na hali iliobadilika na lijizatiti barabara kisilaha.Kwani jambo moja lapasa kufahamika wazi:Kurudishwa nyumbani si jambo linalowezekana mnamo muda mfupi ujao.Na hata ukweli huu hausemwi."
Gazeti la Badische Zeitung kutoka Freiburg laandika kwamba,licha ya mwito wa kushika uzi huo huo na kuzuwia mjadala,kuna hatari ya kuzuka msiba.Gazeti laandika:
"Dhana inazidi kupata nguvu kuwa wanajeshi watakua tu na nafasi ya kutekeleza jukumu waliopewa ,ikiwa juhudi za kuijenga upya Afghanistan ili kuwanufaisha raia zikitanuliwa zaidi.Hili ni swali linalopasa kujadiliwa.
Kwani bila uamuzi wazi msaada kwa raia utakavyokuwa na kwetu sisi una maana gani,basi itakuwa tumewapeleka wanajeshi wetu mtegoni."
Likizungumzia mvutano kati ya kambi ya magharibi na Urusi, gazeti la Cellesche Zeitung laonya:
"Yule asietaka kuja kuonewa na Urusi,anabidi kusaka uwezekano mwengine wa kuachana kutegemea gesi na mafuta kutoka Urusi .
Katika mada hii nyeti si kila mwanasiasa maarufu wa siku za nyuma ni mshauri wa busara kufuatwa.
Likitugeuzia mada ,gazeti la Wetzlarer Neue zeitung lakichambua chama cha SPD na hali yake kinachojikuta wakati huu:
Laandika:
"Hakuna kinachobashiria hivi sasa kuwa wasocial demokrat wamepoteza hamu ya kujitosa binafsi kisimani.Mfano bora ni dai la bawa la mrengo wa shoto la SPD kudai chama kirejee sera zake za zamani za kijamii na za kodi.Kwa njia hiyo kinaamini chama cha SPD au matawi yake kadhaa ya mrengo wa shoto kitawarudisha wapigakura chamani ikiwa wataigiza msimamo wa chama cha mrengo wa shoto cha Bw.Lafontaine.... ?
Gazeti la Rhein-Necker-zeitung lazungumzia kurudi katika uongozi wa chama kwa Bw.Franz Mżnterfering:
"Shangwe zilizoonekana jana alipojitokeza katika kampeni ya uchaguzi mjini Munich,haiwezi kutafsiriwa kweli amerudi kileleni mwa chama.kwani, nafasi hizo za kileleni ambazo angechukua zimeshadhibitiwa na wengine...."