1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Uingereza lapoteza udhibiti wa jimbo la kusini mwa Iraq.

Sekione Kitojo26 Agosti 2007

Majeshi ya Uingereza yaliyoko kusini mwa Iraq yanaonekana kuwa yamepata mafanikio makubwa kuliko wenzao wa Marekani walioko katikati ya nchi hiyo. Lakini kwa hakika majeshi ya Uingereza yanaonekana kupoteza udhibiti huo. Kama anavyoeleza Sabine Matthay katika ripoti yak

https://p.dw.com/p/CB1k

e.

Hatua za ulinzi katika ujenzi mpya wa taifa, ndivyo unavyosema uchambuzi wa taarifa juu ya kuwepo kwa majeshi ya Uingereza katika mwaka wake wa tano kusini mwa Iraq pamoja na ukosoaji mkubwa ambao unatoka Marekani. Waingereza ambao kwa muda mrefu kazi ya ujenzi mpya imekuwa ya mafanikio kuliko upande wa majeshi ya Marekani katikati ya nchi ya Iraq, hivi sasa hali haiko hivyo tena katika eneo lao.

Hali imekuwa taratibu ikiharibika kutokana na kutokea kwa kiasi kama mapigano ya makundi ya kihalifu na kushindwa kwa polisi kudhibiti kiwango cha machafuko. Hali imeanza taratibu kuwa mbaya.

Mapigano ya mara kwa mara ya makundi ya kihalifu, kutokuwa na udhibiti wa ghasia hizo , ndivyo anavyoieleza hali ilivyo jenerali msataafu wa jeshi la Marekani Jack Keane, ambaye ni mshauri wa masuala ya kijeshi wa serikali ya Marekani kuhusu hali kusini mwa Iraq.

Pekee katika mwezi wa August magavana wawili wa majimbo kusini mwa Iraq waliuwawa katika mashambulizi, mji mkuu wa jimbo hilo la kusini Basra umekuwa ukidhibitiwa sasa na makundi hasimu ya Washia, ambayo yamekuwa kila mara yakipigana na majeshi ya Uingereza.

Si hivyo tu, katika mwaka 2004 wanajeshi kumi wa jeshi la Uingereza wameuwawa katika mapigano, wakati katika mwaka huu hadi sasa idadi hiyo imeongezeka maradufu.

Jeshi la Waingereza limekuwa halifanyi chochote, kisiasa hawashughuliki, amesema Anthony Cordesman kutoka katika kituo cha mafunzo ya mikakati ya kimataifa mjini Washington.

Mwanzoni mkakati wa jeshi la Uingereza uliwafurahisha wa Iraq. Wakati wakiwa na kofia za chuma hufanya wanajeshi wa Uingereza doria mitaani na wanajaribu kuwa na mahusiano na raia. Lakini mwanzoni mwa ujenzi wa taifa hilo, ulikuwa umeshaamuliwa, anasema mtaalamu wa masuala ya kisiasa Toby Dodge kutoka katika chuo kikuu cha London.

Amesema kuwa Waingereza tangu mwanzo hawakuwa na wanajeshi wa kutosha, na miundo mbinu, pamoja na uwezo wa kupambana na haya yote. Katika mwaka 2003 / 2004 walikuwa karibu miongoni mwa jamii ya Wairaq kwa kiasi fulani, wakifanikiwa kuweka udhibiti katika ghasia, lakini sasa kazi yao inakuwa kama gari lililokosa breki kutokana na ghasia na mauji yanayotokea Basra.

Kama mshirika wa kampeni dhidi ya Saddam Hussein Uingereza hususan katika mpango ambao umekuwa na makosa wa Marekani , ambao ulikosolewa sana , pamoja na bajeti ndogo ya Uingereza katika uendeshaji wa ujenzi mpya na uratibu mbaya wa ndani na umeathiri sana uwezo wa majeshi ya Uingereza.

Wakati wa uvamizi dhidi ya Iraq mwezi March 2003 kulikuwa na wanajeshi 45,000 wa Uingereza, lakini miezi mitano baadaye wanajeshi hao walikuwa 9,000 tu kusini mwa Iraq.

Hivi leo wako wanajeshi 5,000 tu wa Uingereza walioko nchini Iraq. Sababu ni kupungua kwa majeshi ya Uingereza . Wako wanajeshi 100,000 tu hivi sasa , ikiwa ni idadi ndogo kabisa tangu mwaka 1840.

Jeshi hivi sasa limefikia kikomo, amesema mkuu wa jeshi la Uingereza Sie Richard Dannat , na wakati akisema hivyo amedokeza kuwa hatuwezi kuajiri wanajeshi zaidi wakati huu , ndio sababu alikuwa anajaribu kuwa na uwiano sahihi kati ya muda wa kuweka majeshi, muda wa mafunzo na kuyaweka katika makambi.

Wakati huo huo majeshi ya Uingereza yamepoteza udhibiti wao katika majimbo ya kusini nchini Iraq, wakati huo huo wakiacha kujishughulisha na mapambano na kujichimbia katika kasri la zamani la Saddam Hussein mjini Basra.

Na kwa hiyo wako wanajeshi 5,000 tu mbele ya lango ya lango kuu la uwanja wa ndege wa mji huo, ambapo katika miezi iliyopita walikuwa kila siku wakipambana na makombora ya wapiganaji.

Hivi sasa Waingereza kila siku wanajiuliza , majeshi ya nchi hiyo yatabaki hadi lini na kwa lengo gani.