1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Uganda kujiunga na Congo kuwakabili waasi

13 Mei 2021

Majeshi ya Uganda na Congo yanatengeneza kituo cha operesheni mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa ajili ya kuanzisha operesheni ya pamoja dhidi ya waasi ambao wamewauwa mamia ya watu mwaka jana

https://p.dw.com/p/3tLHQ
Uganda Afrika Soldaten Sicherung Demonstration
Picha: picture-alliance/dpa/D.Kurokawa

Majeshi ya Uganda na Congo yanatengeneza kituo cha operesheni mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa ajili ya kuanzisha operesheni ya pamoja dhidi ya waasi ambao wamewauwa mamia ya watu mwaka jana.

Taarifa ya wizara ya habari ya Congo imesema ujumbe wa jeshi la Uganda - UPDF akiwemo kamanda wa vikosi vya ardhini vya Uganda ulikuwa Beni katika mkoa wa Kivu Kaskazini nchini Congo ili kuunda kituo cha uratibu kwa majeshi ya nchi hizo mbili. Taarifa hiyo imesema bila kufafanua kuwa majeshi ya Congo na Uganda yamedhamiria kupambana na waasi wa ADF.

Mnamo Mei 3 Congo ilitangaza sheria ya kijeshi katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Ituri katika matumaini ya kushughulikia hali inayoendelea kuwa mbaya ya umwagaji wa damu katika jimbo hilo kubwa linalopakana na Uganda