1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Jeshi la Sudan kurejelea mazungumzo ya kusitisha mapigano

15 Julai 2023

Wawakilishi wa jeshi la Sudan wamerejea mjini Jeddah nchini Saudi Arabia kwa mazungumzo na mahasimu wao huku vita kati ya majenerali wawili pinzani vikiingia mwezi wa nne.

https://p.dw.com/p/4Tx6n
FILE PHOTO: Sudan's General Abdel Fattah al-Burhan talks to troops about truce extension
Picha: Sudanese Armed Forces/REUTERS

Taarifa hiyo imetolewa leo na chanzo cha serikali kilichozungumza kwa sharti la kutotambulishwa kwa kukosa idhini ya kuzungumza na vyombo vya habari, Kwa upande wake, kikosi hasimu cha wanajeshi wa dharura cha RSF hakijatoa tamko kuhusu mazungumzo hayo ya Jeddah ambayo wapatanishi wa mazungumzo hayo, Marekani na Saudi Arabia waliahirisha mwezi uliopita baada ya kuendelea kwa mfululizo wa kukiukwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano.

Mashuhuda mjini Khartoum waripoti kuzuka kwa mapigano

Katika hatua nyingine, mashuhuda katika mji mkuu Khartoum, kwa mara nyingine, leo wameripoti kuzuka kwa mapigano siku moja baada ya mapambano makali ya jana Ijumaa yaliosababisha kurindima kwa moshi mweusi katika maeneo kadhaa ya mji huo.