Jeshi la polisi Tanzania kuteketeza silaha haramu
9 Desemba 2021Matangazo
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, msemaji wa jeshi la polisi nchini Tanzania David Misime amebainisha kuwa silaha hizo zimepatikana kwa oparesheni iliyofanywa nchi nzima na jeshi hilo kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama.
Uteketezaji wa silaha hizo unafanyika kwa mujibu wa sheria za Tanzania na kwa kuzingatia mikataba ya kimataifa na kikanda ambayo Tanzania imeridhia, kwa ajili ya kupambana na silaha ndogo na nyepesi kama ilivyoainishwa katika itifaki ya Umoja wa Mataifa.
Jeshi hilo limesema silaha hizo zitateketezwa hadharani ili wananchi washuhudie, na kisha vyuma vitakusanywa na kuandaliwa utaratibu wa kuyeyushwa kwa ajili ya matumizi mengine.