UhalifuAmerika ya Kaskazini
Jeshi Mexico lawauwa watu 12 wenye silaha karibu na Marekani
19 Februari 2024Matangazo
Mamlaka za usalama eneo hilo zimeeleza kuwa majibizano ya risasi yalitokea katika manispaa ya Miguel Aleman kwenye mpaka na Marekani baada ya maafisa kushambuliwa na watu wenye silaha waliokuwa wamejificha msituni. Jeshi la Mexico lilitumia droni na helikopta katika operesheni hiyo.
Soma pia:Watu wapatao 10 wauwawa Ecuador
Tangu kuanzishwa kwa operesheni kabambe ya kijeshi ya kupambana na biashara haramu ya madawa ya kulevya mnamo mwaka 2006, Mexico imeshuhudia visa 420,000 vya mauaji huku karibu watu 110,000 wakitoweka. Idadi kubwa ya matukio hayo yanahusishwa na magenge ya uhalifu.