Jeshi la Libya lakaribia kuitwaa Sirte
23 Novemba 2016Matangazo
Muda mfupi kabla ya kuanza kwa opresheni hiyo ya kuukomboa mji wa Sirte hapo jana (Novemba 22), vidio iliyoonekana katika mitandao ilionyesha wapiganaji wakitumia vipaza sauti kuwahimiza wanawake na watoto kuondoka eneo hilo na kuwaahidi usalama wao wanapoondoka.
Vikiungwa mkono na mashambulizi ya angani ya Marekani, vikosi vya majeshi yanayounga mkono serikali ya Líbya yamekuwa yakipiga hatua dhidi ya wanamgambo wa IS walioko katika eneo hilo lililo karibu na Bahari ya Meditarrania.
IS iliudhibiti mji huo mwaka jana na iwapo jeshi na wapiganaji watiifu kwa serikali watafanikiwa kuukomboa, basi IS itapoteza ngome yake pekee nchini Libya.
Operesheni ya kuukomboa mji huo ilianza tangu mwezi Mei 2016.