Jeshi la Kenya lashiriki katika biashara ya magendo
Saumu Ramadhani Yusuf/M M T17 Novemba 2015
Jeshi la ulinzi la Kenya linaloshiriki katika operesheni ya kupambana na kundi la Itikadi kali nchini Somalia Al Shabaab, limetuhumiwa kuhusika katika biashara ya magendo ya sukari na mkaa nchini humo. Saumu Mwasimba alizungumza na Afisa wa Mawasiliano kutoka wizara ya ulinzi ya Kenya Borgita Ong'eri aliyejibu tuhuma hizo.