1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Israeli lalenga ngome za Hamas huko Gaza

24 Agosti 2021

Jeshi la Israeli limesema kuwa ndege zake za kivita zimezishambulia kwa mabomu ngome za kundi la Hamas katika Ukanda wa Gaza kujibu hatua ya kurushwa kwa maputo yaliyokuwa na vilipuzi kutoka upande wa Palestina

https://p.dw.com/p/3zPx2
Gaza I Israelische Angriffe treffen Punkte der palästinensischen Widerstandsgruppen im Gazastreifen
Picha: Ashraf Amra/AA/picture alliance

Ndege za kivita za Israel zimezilenga ngome kadhaa katika Ukanda wa Gaza usiku kucha na kusababisha ufyetuaji wa risasi kutoka kwa kundi la Hamas katika mapigano makali zaidi ya pande hizo mbili tangu vita vya siku 11 mnamo mwezi Mei. Katika eneo la Ukingo wa Magharibi, maafisa wanasema kuwa kijana mmoja wa Kipalestina aliuawa katika mapigano hayo ya leo na jeshi la Israel.

Mamlaka ya Palestina inasema kuwa kijana huyo aliuawa baada ya kupigwa risasi kichwani wakati wa mapigano hayo katika mji wa Nablus. Jeshi la Israeli limesema kuwa wanajeshi walikuwa wanafanya msako wa kuwakamata watu katika kambi ya wakimbizi ya Baltawalipokabiliwa na ushambuliaji kutoka maeneo ya juu ya majengo yaliyoko karibu.

Palästina | Proteste am Grenzzaun im Gazastreifen
Waandamanaji wajaribu kupanda ukuta wa mpaka kati ya Gaza na IsraelPicha: Adel Hana/AP Photo/picture alliance

Wanajeshi hao wanasema kuwa matofali makubwa yalirushwa kutoka kwenye majengo hayo na kwamba wanajeshi wake wakampiga kwa risasi mwanamume mmoja ambaye wanadai alikuwa anataka kuwarushia kifaa kikubwa, lakini haikubainishwa iwapo kijana huyo aliyetambulishwa kama Imad Hashash alikuwa mtu huyo. Tangu makubaliano ya kusitishwa kwa mapigano ya siku 11 kati ya Israel na kundi la Hamas mnamo mwezi Mei yaliosimamiwa na Misri, wapiganaji wa Gaza wamekuwa wakirusha maputo yenye vilipuzi kuelekea Israel na kuichochea Israel kushambulia taasisi za kundi hilo.

Sababu ya kurushwa kwa maputo ya vilipuzi

Palestina inasema kuwa maputo hayo yanayobeba vilipuzi yanalenga kuishinikiza Israel kulegeza vikwazo dhidi ya Gaza na kuruhusu msaada kuifikia ngome hiyo. Huduma ya uokoaji na ya zimamoto ya Israel imesema kuwa maputo yaliyorushwa jana Jumatatu yalisababisha mioto katika viwanja vya Israeli katika eneo la mpaka wa Ukanda wa Gaza. Vikikabiliana na waandamanaji wa Ukanda wa Gaza hapo jana walioteketeza magurudumu na kurusha vilipuzi katika mpaka huo, vikosi vya Israel viliwafyatulia risasi na kuwajeruhi wapalestina 41 huku wawili wakiwa mahututi. Haya ni kwa mujibu wa maafisa wa matibabu.

Vurugu hizo zinatokea huku mazungumzo ya amani yanayosimamiwa na Misri yakiendelea kufifia. Pia zinatishia kuhujumu mkutano wa kwanza wa waziri mkuu Naftali Bennett katika wadhifa huo na Rais wa Marakani Joe Biden mjini Washinton.